Bawasiri ni ugonjwa unaotokea sehemu ya haja kubwa na ndani ya utumbo mkubwa. Bawasiri inatokea kwa kuvimba mishipa sehemu hizo na kusababisha vinyamanyama kuota sehemu ya mkundu na ndani ya utumbo mkubwa.

Hivyobasi bawasiri imegawanyika katika aina mbili,

  • Bawasiri ya ndani: Hii ndio ile inayotokea ndani ya utumbo mkubwa
  • Bawasiri ya nje: Hii ndio ile inayotokea kwa kuota vinyamanyama sehemu ya haja kubwa.

Bawasiri ni ugonjwa wa kawaida kwa watu wazima. Watu wengi sana wakishafika umri mkubwa huwa wanapata tatizo hili. Tafiti zinaonyesha kuwa watu wazima watatu kati ya wanne wanaumwa ugonjwa huu.

Uzuri ni kwamba ugonjwa huu unatibika endapo utafata masharti ya matibabu na maelekezo utakayo pewa kuhusu dawa zake.

Dalili za Bawasiri

Kama nilivyosema mwanzo bawasiri ipo ya aina mbili. Kuna bawasiri ya nje na ya ndani. Hivyo hapa tutaanza kuanisha dalili za bawasiri ya nje kisha tutamalizia na za ndani

Bawasiri ya Nje

  • Muwasho sehemu ya haja kubwa
  • Uvimbe au kuota kwa vinyamanyama sehemu ya haja kubwa
  • Kutokwa kwa damu wakati wa kujisaidia
  • Kupata maumivu sehemu ya haja kubwa

Bawasiri ya Ndani

  • Kutokwa kwa damu wakati wa kujisaidia. Hali hii huwaga haiambatani na maumivu yoyote.
  • Kutokwa na madonge ya nyama laini ilioambatana na damu wakati wa kujisaidia

Sababu zinazosababisha ugonjwa wa bawasiri

  • Unene
  • Umri mkubwa
  • Kutumia nguvu nyingi sana kubeba vyuma kwa mda mrefu
  • Kukaa mda mrefu chooni wakati wa haja kubwa
  • Kutumia nguvu nyingi kusukuma kinyesi
  • Kula nyama kwa wingi
  • Kukosa vyakula vya mboga za majani
  • Kuharisha kwa mda mrefu
  • Kufanyiwa mapenzi kinyume na maumbile
  • Mimba

Hatari za kuwa na Bawasiri

  • Kansa ya damu: Bawasiri isipotibiwa inaweza sababisha kansa ya damu ambapo itaanzia kwenye utumbo mkubwa kisha kuja kwenye damu mwili mzima.
  • Vimbe ngumu kwenye sehemu ya utumbo mkubwa: Ugonjwa huu ukizidi kwa mda mrefu, utumbo mkubwa huathirika kwa kupata vimbe ngumu ngumu kwenye kuta zake
  • Kuvilia kwa damu: Damu inaweza kuvilia sehemu ya haja kubwa na kufanya mtu apate maumivu makali sana. Hii hali huwa mtu anapata mda wote wa kujisaidia haja kubwa au hata akiwa amekaa.

Dawa ya bawasiri na njia za kujikinga

Bawasiri hutokea kwa sababu kuu ya kupata choo kigumu. Kwaio chochote kile ambacho kitapelekea kupata choo kilaini kitakuepusha na ugonjwa huu. Vifatavyo ni baadhi ya vitu vya kufanya kujiepusha au kutibu ugonjwa huu

  • Kunywa maji kwa wingi: Maji husaidia kulainisha choo.
  • Kula matunda: Matunda kama mapapai, ndizi, parachichi unashauriwa kula kwa wingi.
  • Mboga za majani: Mboga za majani zina fibre kwa wingi na husaidia mmengenyo wa chakula mwilini. Hivyobasi ni muhimu kwa mtu mwenye tatizo la bawasiri
  • Mazoezi: Ukifanya mazoezi inasaidia kuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini na chakula kumengenywa vizuri.
  • Usijikamue wakati wa haja kubwa: Jitahidi uwezavyo kutotumia nguvu wakati wa haja kubwa. Hii husaidia kuepusha mishipa kutopasuka na kuleta vidonda sehemu ya haja kubwa
  • Usikae mda mrefu chooni: Kukaa mda mrefu huchangia mishipa kupasuka maana inakua imetanuka kwa mda mrefu. Hivyo basi washauriwa kwenda chooni mapema pale unapojisikia kupata haja na kutoka mapema endapo ushatoa kinyesi kilichokua kinakusumbua kwa mda huo. Si lazima umalize kinyesi chote kwa pamoja. Unaweza punguza mda kwa mda hii njia inasaidia sana

Kuhusu dawa

Kwa tiba ya haraka na uhakika zaidi bila kufata masharti. tumia dawa kutoka page hii

DAWA YA BAWASIRI SUGU