Vidonda Vya tumbo ni vidonda ambavyo hutokea ndani ya utandu wa utumbo na sehemu ya juu ya utumbo mdogo. Dalili yake kubwa ni maumivu ya tumbo
Vidonda vya tumbo vipo vya aina mbili
- Inatokea ndani ya tumbo
- Inatokea kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo
Chanzo chake ni nini?
Vidonda vya tumbo husababishwa na bakteria aitwae Helicobacter Pylori (H.Pylori) pamoja na matumizi ya mda mrefu wa dawa za kupunguza maumivu ya mwili kwa ujumla kama panadol badala ya dawa hususani kwa ajili ya tumbo. Msongo wa mawazo na vyakula vya viungo vikali kama pilipili sio chanzo cha huu ugonjwa ingawa kama umesha athirika vinachochea ugonjwa huu.
Dalili za Vidonda vya tumbo
- Kiungulia
- Tumbo kujaa gesi
- Kushindwa kula vyakula vya mafuta
- Kuhisi mda wote umeshiba
- Kichefuchefu
- Inatokea kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo
Jinsi ya kujikinga na Vidonda vya tumbo
Kama umeshajigundua unadalili za vidonda vya tumbo, ni vyema ukifata masharti haya ili kupunguza athari za vidonda kuongezeka.
- Sigara: Sigara inachochea bakteria wa H.pyroli kwa mtu ambaye ameshapata bakteria hawa
- Pombe: Inaondoa kamasi za tumboni hivyo huongeza acid tumboni ambayo inaenda athiri vidonda ulivyo pata na kufanya viongezeke.
- Msongo wa mawazo
- Vyakula vya viungo vikali kama pilipili
Madhara ya vidonda vya tumbo visipo tibiwa
- Kuvuja damu ndani kwa ndani: Hii inaweza kutokea katika mwili na kusababisha upungufu wa damu, Dalili kubwa ya kuvuja damu ni kujisaidia choo cheusi au choo chenye damu nyeusi au kutapika damu au vitu vyeusi.
- Kupata tundu tumboni: Ugonjwa wa vidonda vya tumbo unaweza ukazidi kwa kukwangua tumbo mpaka kuleta tobo kwenye tumbo. Hii ni mbaya zaidi kwa tumbo.
- Kushindwa kula: Vidonda hivi vinaweza sababisha ukashindwa kula kabisa au kutapika endapo utajaribu kula. Hali hii hupelekea kupungua kwa uzito
- Kansa ya Utumbo: Watu wengi wenye vimelea vya H.pyroli wameonekana wakipata kansa ya utumbo endapo hawajatibiwa.
Maziwa na Vidonda vya tumbo
Watu wengi huwa wanashauriana kutumia maziwa kama moja ya dawa ya vidonda vya tumbo, hili jambo si kweli. Maziwa yanasaidia kutengeneza ute wa kamasi kwenye tumbo kwa muda mfupi baada ya hapo hupotea. Maziwa ni mabaya zaidi maana huchochea kutengenezwa kwa acid ndani ya tumbo ambayo kama endapo unavidonda vya tumbo lazima utaumia na kuviongeza.
Hivyo basi kama unajua unavidonda vya tumbo au dalili za vidonda vya tumbo usitumie maziwa aina yoyote iwe fresh au mtindi/mgando